<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><hymn_number>60</hymn_number>
<title>Waponyeni Watu TZR60</title>
<lyrics>[V1]
 Waponyeni watu wamo kifoni,
 Watoeni walio shimoni;
 Na aangukaye mumzuie;
 Ya Bwana Yesu wahubirini.

[V2]
 Walio kifoni waokoeni,
 Mwokozi yuko, wahubirini.

[V3]
 Wajapokawia anangojea,
 Awasubiri waje tobani;
 Msiwadharau, muwaonyeni;
 Huwasamehe; wakiamini.

[V4]
 Myoyoni mwa ndani, yule shetani
 Ameyaseta mawazo yao;
 Lakini kwa Bwana huwa mazima,
 Tukiwavuta kwa pole hao.

[V5]
 Kawaokoeni, wale njiani,
 Mutimize mapenzi ya Bwana;
 Na kwa nguvu zake warudi kwake,
 Kwa subira waonyeni sana.</lyrics>
</song>